The House of Favourite Newspapers

Mainda Adaiwa Kukimbia Kwake, Aishi kwa Muna!

Muna.

DAR ES SALAAM: Ubuyu mtamu wa Wikienda! Kumeibuka ubuyu matata wa staa wa kitambo wa maigizo Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ akidaiwa kukimbia nyumbani kwake, Kijitonyama, Dar na kwenda kuishi nyumbani kwa mwigizaji mwenzake, Rose Alifonce ‘Muna Love’ maeneo ya Mbezi-Beach, Dar.

Ruth Suka ‘Mainda’.

Mtoa ubuyu wetu aliliambia Wikienda kuwa, chanzo cha yote ni madai ya Mainda kukosa kodi ya kulipia nyumba aliyokuwa anaishi maeneo ya Kijitonyama, Dar kwani kwa sasa hafanyi kazi yoyote kuanzia kuigiza hadi biashara.

ADAIWA KUJIFICHA

Katika ishu hiyo, Wikienda lilinyetishiwa kuwa, Mainda siku hizi anaishi kwa Muna na kila mgeni akifi ka nyumbani hapo, kama hahusiani na nyumba hiyo, Mainda hujifi cha ili asionekane.

“Hivi jamani Wikienda mna ubuyu? Basi ubuyu mubashara unanyetisha kuwa, Mainda anaishi kwa Muna na wageni wakifi ka huwa anakimbilia chumbani kuepuka maneno? Anaishi bila raha kwani ukienda kwa Muna, utamkuta amejaa tele,” alisema sosi huyo.

MAINDA ASAKWA

Baada ya ubuyu kumung’unywa, Wikienda lilimsaka Mainda kwa njia zote za simu na mguu kwa mguu, lakini halikufanikiwa kumpata ndipo likamtafuta Muna ili kupata ukweli wa ubuyu huo na kubaini kuwa lisemwalo lipo.

MUNA AMFUNGUKIA MAINDA Muna, alipoulizwa juu ya ishu hiyo, alianza kwa kusema:

“Mainda mbona  anaishi nyumbani kwake maeneo ya Hongera (Kijitonyama) pale anapoishi siku zote? Ukimsaka utampata. Katika mazungumzo na Wikienda, Muna alisema kuwa, Mainda ni ndugu yake (hakutaka kufafanua kivipi) na amekuwa akiishi nyumbani kwake (kwa Muna) pale anaposafiri kwa sababu huwa hakuna mtu mzima wa kumuachia nyumba ndiyo maana huonekana kwake mara kwa mara.

“Unajua watu wanapenda sana kuongea. Mainda anaishi nyumbani kwake na huwa anakuja nyumbani kwangu kama mimi nikisafiri. Unajua watu wengi hawajui kuwa Mainda ni ndugu yangu na anakuja kwangu wakati wowote anaohitaji,” alisema Muna.

Hata hivyo, Muna alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mainda kutotaka kutoa ushirikiano, hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwani kumekuwa na madai ya muda mrefu kuwa msanii huyo sasa anaishi kwa Muna tena kwa kujifi cha kwani watu wakifi ka nyumbani hapo hujificha.

NENO LA MHARIRI

Huenda Mainda ameamua kuishi kwa ndugu yake na si tatizo, lakini mashabiki wake wamekuwa wakilalamikia ukimya wake hasa kunapokuwa na ubuyu kama huu wakihitaji kumuona akijitokeza na kutolea ufafanuzi lakini hata hivyo tunazingatia msemo wa mtu hapangiwi cha kufanya bali anapanga yeye anachokitaka.

Iwapo Mainda atapatikana na kufunguka, tunaahidi kuwaletea kile atakachokisema kupitia ukurasa huu wa ubuyu kwani jitihada za kumuweka ‘mtukati’ zinaendelea.

Comments are closed.