The House of Favourite Newspapers

Wadau Wa Afya watakiwa kupambana kuimarisha Afya ya Mama

0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wanahabari.
Rais wa AGOTA Prof. Andrea Barnaba Pembe akiongea jambo.
Wakiwa katika picha ya pamoja.

Wadau Wa Afya watakiwa kupambana kuimarisha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto.
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wametakiwa kufanya juhudi katika kuimarisha afya ya mama mjamzito na mtoto nchini ili kupunguza idadi ya vifo na kujenga taifa imara.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 24 wa Wanasayansi wa (AGOTA) uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri ummy amesisitiza kuwa vifo kwa wanawake wenye ujauzito bado ni tatizo sugu nchini, ambalo linahitaji jitihada na nguvu zaidi kupambana nalo ili kutokomeza kabisa tatizo hilo Tanzania.
“Naishukuru taasisi ya AGOTA kwa jitihada inazofanya ikiwemo kuhamasisha uzazi wa mpango,kufanya tafiti mbali mbali, kushauri na utoaji huduma ya Afya kwa mwanamke” alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Rais wa AGOTA Prof. Andrea Barnaba Pembe ametoa pongezi kwa Waziri Ummy Mwalimu kutokana na jitihada anazoendelea kufanya kupitia Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi hiyo.

Leave A Reply