The House of Favourite Newspapers

Tetesi za Usajili Bongo, Chuji Ajiweka Sokoni

0
Kiungo wa zamani wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’.

Chuji ajiweka sokoni
KIUNGO wa zamani wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’ amefunguka kuwa yupo tayari kujiunga na timu yoyote kufuatia kumaliza matatizo yake ya kifamilia. Chuji ambaye aliwahi kuzitumikia Yanga, Simba na Mwadui, hakuweza kuonekana msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara licha ya kuwa miongoni mwa wachezaji wakongwe walioipandisha Mwadui misimu mitatu iliyopita. Chuji ameliambia Championi Jumatano kuwa, kwa sasa yupo tayari kufanya kazi na timu yoyote itakayompa ofa ya maana kujiunga nao kwa ajili ya msimu ujao kwani sasa yupo fiti baada ya kumaliza matatizo ya kifamilia yaliyomfanya asionekane msimu uliopita.

Kiungo Simba kuzamia Serbia
KIUNGO wa Simba, Hija Ugando, kwa msimu ujao anaweza asionekane ndani ya kikosi hicho baada ya kupata dili la kucheza soka kwenye moja ya timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Serbia. Meneja wa kiungo huyo, Jamal Kisongo, ameliambia Championi Jumatano kuwa, mchakato wa Ugando kutimkia nchini humo unaenda freshi na muda wowote kutoka sasa anaweza kukwea pipa kwa ajili ya kuelekea huko. “Ugando amepata ofa kutoka Serbia ambapo kuna timu ya huko imemtaka ambapo kwa sasa nafanya mipango ya kuhakikisha nalifanikisha suala la yeye kwenda kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya kuichezea kwa msimu ujao,” alisema Kisongo

Mmalawi wa Mbeya amvuta Rasta wa Madini
KIUNGO mshambuliaji wa Madini FC ya Arusha, Awesu Awesu ‘Rasta’ yupo kwenye mazungumzo ya kutimkia ndani ya kikosi cha Mbeya City kinachonolewa na Mmalawi, Kinnah Phiri kwa ajili ya kukipiga katika msimu ujao wa ligi. Awesu aliyekuwa anawindwa na Simba, ameliambia Championi Jumatano kuwa, ameamua kutimkia Mbeya City kutokana na timu za Simba na Singida United zilizomfuata awali, kushindwana naye. “Kwa sasa naongea na Mbeya City baada ya kuona dili za kuhamia Simba na Singida United kufeli, kila kitu kinakwenda vyema na siku si nyingi nitadondoka saini kujiunga na kikosi hicho,” alisema.

Beki Mbeya City aamua kusepa
EKI kisiki wa Mbeya City, Tumba Sued, ameweka bayana kuwa yupo kwenye mchakato wa kukihama kikosi hicho baada ya kumaliza mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo aliyojiunga nayo akitokea Coastal Union ya Tanga. Tumba ameliambia Championi Jumatano kuwa, kwa sasa anasaka timu nyingine ya kuichezea baada ya mkataba wake kufika ukingoni huku malengo yake ni kwenda kucheza soka la kulipwa nchi za nje. “Mimi nipo huru kwa sasa baada ya kumaliza mkataba wangu na Mbeya City tangu nilipojiunga nayo nikitokea Coastal Union ambapo nazikaribisha timu zinazonitaka tuje tufanye mazungumzo japo kipaumbele changu cha kwanza ni kusaka timu nje ya Bongo,” alisema.

Leave A Reply