The House of Favourite Newspapers

SIMBA WATUA DAR ES SALAAM KUTOKA SAUZI, WAPO KAMILI KWA SIMBA DAY

1
SIMBA WATUA DAR ES SALAAM KUTOKA SAUZI WAPO KAMILI
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya timu hiyo kuwasili nchini ikitokea Afrika Kusini, jana Jumamosi.

Baada ya kufanya mazoezi kwa siku kadhaa nchini Afrika Kusini hatimaye  wakijiandaa kwa ajili ya msimu ujao wa 2017/18, hatimaye kikosi cha Simba kimerejea salama jijini Dar.

SIMBA WATUA DAR ES SALAAM KUTOKA SAUZI WAPO KAMILI
Dokta wa Simba, Yasin Gembe (kushoto) akiwa na Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Idd Kajuna

Simba ambayo ilikuwa Sauzi kuweka kambi ikiwa na wachezaji wake wapya kasoro Haruna Niyonzima, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki katika Tamasha la Simba Day litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Jumanne ijayo Agosti 8 dhidi ya Rayon Sports.

SIMBA WATUA DAR ES SALAAM KUTOKA SAUZI WAPO KAMILI
Kiungo wa Simba, James Kotei akiwa ndani ya basi lao muda mfupi baada ya kuwasili nchini

Wachezaji wa timu hiyo waliwasili kwa mafungu ambapo hali hiyo ilitokana na kupata tiketi katika ndege tofauti.

Katika tamasha hilo, Simba inatarajiwa kumtambulisha mchezaji wake mpya Haruna Niyonzima ambaye hakuwepo kambini kutokana na masuala ya kifamilia aliyokuwa akiyaweka sawa nchini Rwanda ambapo ni nyumbani kwao.

SIMBA WATUA DAR ES SALAAM KUTOKA SAUZI WAPO KAMILI
Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog akiwa uwanja wa ndege muda mfupi baada ya kuwasili.
1 Comment
  1. […] cha Simba leo kimefanya mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterani uliopo Ununio jijini Dar ikiwa ni maandalizi […]

Leave A Reply