The House of Favourite Newspapers

CUF ya Maalim Watoa Kauli Nzito kwa Wabunge wa Lipumba -Video

0
Prof. Ibrahim Lipumba na Maalim Seif.

VIONGOZI wa Chama cha Wananchi (CUF) wametoa kauli nzito kuhusu wabunge wa chama hicho wanaomuunga mkono Mwenyekiti anayetambulika na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba wakidai kuwa wabunge hao ‘wameokotwa vichochoroni’.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zuio la wabunge walioteuliwa na Lipumba kuapishwa, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa CUF, Mbarala Maharagande amedai kuwa, mahakama haikuruhusu wala kukataza kuapishwa kwa wabunge hao licha ya bunge kuwaapisha jana Jumanne mjini Dodoma.

Mbali na hivyo pia wameeleza kutofurahishwa kwao na kitendo cha wabunge wa CCM kuwashangilia wabunge wa CUF ya Lipumba huku wakikiita kitendo hicho kuwa ni njama za CCM kuwatengeneza upinzani feki. Wamedai kuwa lengo la upinzani ni kuikosoa serikali tawala na sio kuipongeza wala kuishangilia.

Aidha wametoa kasoro, wakidai wabunge waliowekwa na Lipumba wameokotwa vichochoroni na kitendo hicho ni uhuni.

Amesema Baraza Kuu la Uongozi la CUF linaendelea kuwatambua wabunge na madiwani waliovuliwa uanachama kwa kuwa bado ni wanachama halali wa chama hicho.

Maharagande amemtupia lawama Spika Job Ndugai akidai analitumia Bunge vibaya kukandamiza upinzani. Amesema bunge linapaswa kuwa chombo muhimu cha Watanzania katika kuisimamia Serikali ili wananchi wapate maendeleo.

Spika Ndugai jana aliwaapisha wabunge saba wa viti maalumu ambao ni Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.

Hindu Mwenda, ambaye pia alikuwa aapishwe jana alifariki dunia Ijumaa Septemba Mosi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa Jumapili Septemba 3.

Wakati wabunge wa upinzani wakisusia, waliohudhuria ni wabunge wa CUF Magdalena Sakaya wa Kaliua, Maftah Nachuma (Mtwara Mjini) na Maulid Mtulia (Kinondoni).

 

SHUHUDIA VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply