The House of Favourite Newspapers

Spoti Xtra Laendelea Kukimbiza Mtaani

Msomaji akifurahia gazeti la michezo la Spoti Xtra leo Chanika, Ilala, Dar es Salaam.
…Akipewa zawadi na msambazaji wa magazeti.
Msomaji akionyeshwa uhondo uliomo katika Spoti Xtra huko Chanika.
Ofisa Masoko, Jimmy Haroub, akimwonyesha msomaji utamu wa Spoti Xtra huko Chanika.
Mkazi wa Chanika aliyenaswa na kamera yetu akisoma Spoti Xtra.
Msomaji wa Chanika akionyeshwa makala ya rekodi za Manchester City iliyotoka katika ukurasa wa katikati wa Spoti Xtra. na habari mbalimbali zilizomo katika Spoti Xtra.
Msomaji wa Chanika aliyenaswa na Spoti Xtra akilisoma kwa makini.
Kamera ya Spoti Xtra iliwanasa wasomaji hawa wakibishana kuhusu habari ya Sanches alivyopotea Manchester United katika ukurasa wa 18.

TIMU nzima ya promosheni ya Gazeti la Spoti Xtra, leo Jumapili kama kawaida iliingia mtaani ambapo ilipofika mitaa ya Chanika nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ikakutana na mapokezi makubwa.

Katika hali ambayo ilionyesha wazi kwamba wasomaji wamekuwa wakilifuatilia na kulisoma Gazeti la Spoti Xtra, wakazi wa eneo hilo walionekana wakiligombania, kwa kila mmoja akitaka kopi ili apate uhondo uliomo ndani.

Wafanyabiashara, wapita njia na wengineo, kwa nyakati tofauti, walionekana wakilisoma gazeti hilo  ambalo hutoka kila Jumapili.

Katika promosheni hiyo, wasomaji waliendelea kujizolea zawadi za sabuni kwa kila aliyekutwa akilisoma.

Comments are closed.