The House of Favourite Newspapers

Mwambusi Apata Timu Ghana, Agoma

Kocha Msaidizi wa Azam, Juma Mwambusi.

TANZANIA ina upungufu wa makocha wazawa wanaofundisha soka nje ya nchi lakini juzikati Kocha Msaidizi wa Azam, Juma Mwambusi alipewa dili la kwenda kuinoa klabu ya huko Ghana lakini akachomoa.

 

Mwambusi amejiunga na Azam kwa mkataba wa miaka miwili kama kocha msaidizi chini ya Mholanzi Hans Der Pluijm ambaye pia aliwahi kuwa na Yanga.

 

Mwambusi ameliambia Championi Jumamosi kuwa, Pluijm aliwahi kupata dili la kuinoa klabu moja nchini Ghana alinitaka niende kufanya kazi huko lakini nilikataa kwa kuwa nilihitaji kupumzika zaidi.

 

“Nimekuwa nikifanya kazi vizuri na Pluijm tangu tulipokuwa Yanga na ni Mzungu wa kwanza kufanya naye kazi, tumekuwa tukielewana kwa kuwa tunashauriana na kukubaliana.

 

“Kuna wakati alipata timu nchini Ghana na kunihitaji nikafundishe lakini sikuwa tayari kwenda na hata alivyoitwa Singida United msimu ulioisha aliniita tukafanye kazi pamoja, lakini nilikataa kwa kuwa nilihitaji kupumzika, kwa sasa nimeona ni muda muafaka wa kuungana naye hapa Azam,” alisema Mwambusi ambaye alikuwa kuinoa Prisons na Mbeya City.

Stori: Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Comments are closed.