The House of Favourite Newspapers

TFF Yamvua Sanga Uenyekiti Bodi Ya Ligi

Rais wa shirikisho la soka nchini (TFF), Wallace Karia (katikati),  akiongea na wanahabari leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred.

KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kilichofanyika leo Julai 12,2018,  makao makuu ya shirikisho hilo, kimemuondoa  aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), Clement Sanga,  kwenye nafasi hiyo kwa kukosa sifa baada ya klabu ya Young Africans kuthibitisha Yusuph Manji kuwa ndiye mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakati huohuo, Kamati ya Uchaguzi  ya TFF imeelekezwa kuandaa uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia,  amesema  hatua hiyo imefuatia mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga ambao ulitamka kuwa bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.

Kamati imepitisha kanuni za kuruhusu usajili wa idadi ya wachezaji 10 wa kigeni katika Ligi Kuu kuanzia msimu ujao.  Wachezaji hao wanaweza kutumika wote kwa wakati mmoja,

Pia, Kamati ya Utendaji ya TFF imemthibitisha Wilfred Kidao kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo.

 

 

Comments are closed.