The House of Favourite Newspapers

Stand United Yafyeka Saba

KATIKA kuhakikisha inakuwa imara Stand United imeachana na wachezaji wake saba na kumsajili kiungo mmoja kutoka Mbeya City, Majaliwa Mbaga.

Wachezaji hao wameondoka Stand United kwa sababu mbalimbali katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

 

Mwenyekiti wa Stand, Erison Maheja alisema wachezaji wao saba wanaondoka ndani ya kikosi hicho na wamesajili kiungo mmoja hadi sasa.

 

“Wachezaji saba ndani ya kikosi chetu tunaachana nao lakini ambao mpaka sasa tumeongea na kuweza kumalizana nao ni pamoja na Erick Mlilo, Musa Kilungi, Juma Ally na Juvenile Pastory na sababu za kuondoka baadhi wameondoka ili wakapate nafasi ya kucheza wengine wameamua kubadili tu mazingira kwa hiari yao wenyewe,” alisema Maheja.

STORI: MARTHA MBOMA,

Comments are closed.