The House of Favourite Newspapers

NMB YATOA MSAADA WA VITANDA, MASHUKA ZANZIBAR

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud (katikati) akimkabidhi  Kitanda na Mashuka Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Ali Salum (kulia).
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi akimkabidhi Mashuka na Kitanda Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia).
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Abdalla Duchi akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa Vitanda vinane (8) na mashuka mia moja na ishirini (120) kwaajili ya Hospitali hiyo.
Mbunge wa viti Maalum Wanawake CCM Asha Abdalla Juma (Mshua) na Mdau wa mambo ya afya akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Vitanda na Mashuka.

 

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda maalum vya kujifungulia pamoja na mashuka katika Hospitali ya Mnazi mmoja, mjini Zanzibar vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 10. Vifaa hivyo vimepokelewa na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Comments are closed.