The House of Favourite Newspapers

Rostam Azizi aomba Radhi kwa Matamshi Aliyoyatoa kuhusu Majaji wa Tanzania

0

Mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Rostam Azizi hii leo amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kauli yake ambayo aliitoa mnamo Juni 26, mwaka huu kuhusu majaji wa Tanzania, huku akiomba radhi kwa yeyote aliyekwazika na kauli zake kwa kusema ilikuwa ni kuteleza kwa ulimi tu lakini dhamira yake haikuwa kutamka maneno hayo na badala yake ilikuwa ni kuuelimisha umma juu ya uwekezaji na namna ambavyo inabidi ufanyike kwenye nchi husika.

Hii imekuja mara baada ya kuona tamko na la Umoja wa majaji na mahakimu hapa Tanzania wakimtaka kutoa uthibitsho kuhusu kauli yake ambapo alinukuliwa akiituhumu Mahakama ya Kisutu kwa kutokuwa huru katika uendeshaji wa shughuli zake.

Kupitia taarifa yake JMAT imeuhabarisha umma kwamba hakuna Jaji anayehudumu katika Mahakama hiyo kama ilivyoripotiwa na mzungumzaji wa taarifa hiyo.

Aidha Chama hicho kimebainisha kuwa Mahakama ya Tanzania ni chombo pekee cha utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au chombo chochote.

Leave A Reply