The House of Favourite Newspapers

ALAF Limited Yazindua Mradi Wa Mtambo Wa Mabati Ya Rangi Wenye Thamani Ya Mabilioni

0
Naibu Waziri Mkuu, Mh Dk. Dotto Biteko (kushoto), akikata utepe kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Mtambo mpya wa mabati ya rangi Alaf Limited Jijini Dar es Salaam huku viongozi wengine na WA kiserikali na Alaf wakishuhudia.

Dar es Salaam Jumapili Oktoba 15, 2023: Kampuni ya ALAF Limited, ambayo ni sehemu ya makampuni ya Safal Group na mtoa huduma bora wa huduma za ujenzi nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, imezindua mradi wa mabati ya rangi wenye thamani ya mabilioni ya shilingi unaolenga kuokoa Zaidi ya dola milioni 190 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi huo mkubwa ilihudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mh. Dk Doto Biteko pamoja na uongozi wa juu wa kampuni ya ALAF Limited, wateja na wadau mbalimbali.

Akiongea katika hafla hiyo, Naibu Waziri Mkuu Biteko aliipongeza Kampuni ya ALAF Limited kwa kuwekeza katika mradi huo mkubwa ambao alisema utaendelea kuiimarisha kampuni hiyo inayojihusisha na uzalishaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi sambamba na kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za chuma bora kwa ajili ya shughuli za ujenzi.

“Hili ni jambo la kupongezwa kwasababu inaonesha dhamira ya dhati mliyonayo ALAF limited katika kumthamini mtanzania kwa kuwafanya kuwa kipaumbele chenu, kuwapa kilichobora kwa maendeleo ya familia, miji na taifa kwa ujumla,” alisema.

Naibu Waziri Mkuu alisema uwepo wa uwekezaji mkubwa kama huu ni matokeo ya jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh Dtk. Samia Suluhu Hassan, katika kufungua milango, kuweka mazingira bora na rafiki kwa wawekezaji kufanya biashara kwa uhuru zaidi. “Uwekezaji wa nanmna hii ni wa kupigiwa chapuo kwakua unawekezwa Tanzania kwa manufaa ya watanzania,” alisema.

Alisema uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni 25 unaonesha ni kwa namna gani sekta ya viwanda hasa uzalishaji na uongezaji wa thamani unavyokuwa kwa kasi.

Alieleza kuwa  pia uwekezaji huu unatoa taswira njema ya Tanzania ijayo namna itakavyokuwa shindani katika soko la ndani na la nje huku Tanzania ikipunguza utegemezi wa bidhaa za nje kunakotokana na kutokutosheleza kwa bidhaa za ndani.

Mh Dk Biteko alitoa changamoto kwa wadau wengine wa sekta ya uzalishaji wa mabati kuamka na kuwekeza kwa ukubwa, ushindani huu utatoa faida kwa mlaji kwa kupata bidhaa bora kwa gharama nafuu.

“Nimedokezwa hapa teknologia itakayotumika hapa ni ya kisasa sana Afrika na hata duniani. Jambo hili linatuhakikishia upatikanaji wa bidhaa bora na za kisasa zaidi , zitakazozalishwa kwa ufanisi mkubwa, gharama kidogo. Hatua hii itatuhakikishia  uchumi endelevu na nguvu ya ushindani kwenye masoko ya kimataifa,” alisema.

Naibu Waziri Mkuu pia alibainisha kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo, ALAF itatengeneza na kusambaza bidhaa zingine za karatasi zinazotumika kwenye miradi ya ujenzi ambazo alosiema zitanakshiwa kwa rangi kupitia mradi huo hivyom kuokoa fedha nyingi za kigeni kutokana na ukweli ya kuwa karatasi aina hizo kwa sasa zinaagizwa kutoka nje ya nchi.

“Nimetaarifiwa ya kuwa, kwa kutengeneza bidhaa hii ndani hapa nchini, Taifa linatarajiwa kuokoa fedha za kigeni zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 190 katika kipindi cha miaka mitano ijayo ambazo zingetumika kuagiza bidhaa hizo nje yan chi”, alisema Dk Biteko.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa ALAF Limited Ashish Mistry alisema mradi huo unaokadiriwa kugharimu dola milioni 25 na ambao uzalishaji wake kibiashara unatarajiwa kuanza Desemba 2024, unalenga kuimarisha miundombinu ya kiwanda kilichoko sasa ili kiwe na mwonekano wa kisasa.

“Lengo kuu la mradi huu ni ujumuishaji mradi wa kuweka nakshi bidhaa za chuma zinazozalishwa hapa nchini ikiwa ni sehemu ya mpango kabambe wa kampuni yetu”, alisema na kuongeza, mradi pia umelenga kutoa huduma za kuweka nakshi ya rangi kwa bidhaa za chuma zikiwemo zile zinazotumika kwenye vyombo vya majini kwa kuzingatia changamoto za kimazingira yaliyoko maeneo ya pwani ya Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alibainisha zaidi kuwa moja wapo ya vipengele muhimu katika mradi huo wa mabati ya rangi ni kuhakikisha hauathiri mazingira na ili kufikia azma hiyo, uongozi utatumia malighafi ambazo hazitaathiri mazingira kwa namna yoyote ile.

“Mradi huu pia umelenga kusisitiza dhamira ya kampuni yetu katika kuzingatia ubora wakati wa kutekeleza majukumu mbalimbali huku tukitoa kipaumbele kwa maswala yanayohusiana na   usalama,  mafanikio endelevu na ubora wa kiutendaji kwa ujumla,” alisema na kuongeza kuwa mradi huo utazalisha ajira za ziada 30 ambazo zitakuwa ni za moja kwa moja na nyingine 250 zisizo za m oja kwa moja”, alisema.

Kupitia mradi huu mpya, ALAF, ambayo ilianza kufanya shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1960, imekuja na suluhisho kamili kwa ajili ya shughuli za ujenzi ambazo hujumuisha bidhaa za kuekeza  kwenye paa zilizopakwa rangi, Pamoja na bidhaa zingine kama yakiwemo mabomba aina mbalimbali yanayotumika kwenye shughuli za ujenzi.

Leave A Reply