The House of Favourite Newspapers

Kukosa usingizi kwa wajawazito (INSOMNIA)

Attractive couple having an argument on couch at home in the living room
Attractive couple having an argument on couch at home in the living room

Insomnia ni tatizo linalowasumbua watu wengi, ambapo hupoteza usingizi, huona maruweruwe na wakati mwingine kuweweseka nyakati za usiku. Hata hivyo, tatizo hili linatajwa kuwa kubwa zaidi kwa wanawake ambapo utafiti wa kitaalamu unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 78 ya wanawake wajawazito hupatwa na tatizo hili.

Chanzo kikubwa cha Insomnia kinatajwa kuwa ni kubadilika utendaji kazi wa mfumo wa homoni mwilini, tatizo ambalo husababisha madhara kwenye ubongo na kuvuruga utaratibu wa kawaida wa usingizi.

Chanzo kingine cha tatizo hili, kinatajwa kuwa ni hofu au matarajio wanayokuwa nayo wajawazito kuhusu kiumbe walichokibeba tumboni kama kitatoka salama au la, msongo wa mawazo, mabadiliko yanayosababishwa na ujauzito na sababu nyingine kadhaa.

Vyanzo hivi na vingine, husababisha mhusika akose usingizi, hata akipata anashtuka mara kwa mara, wakati mwingine akilala anaona maruweruwe au anakuwa usingizini lakini anahisi kama yupo macho.

Katika hatua za awali, Insomnia huwa haina madhara yoyote kwa mama wala mtoto lakini tatizo hilo linapokuwa sugu, huanza kumuathiri mhusika na huweza hata kusababisha mama mjamzito akapata kichaa kama hatapata matibabu mapema.

Pia mama mjamzito asipopata matibabu mapema, ana uwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto aliyepoteza maisha akiwa tumboni, au kusababisha mwanamke mwenyewe akapata matatizo wakati wa kujifungua.

Comments are closed.