The House of Favourite Newspapers

Droo Ndogo ya Tatu Pikipiki ya Tatu Kubebwa Kesho

0
Mr Shinda Nyumaba akitoa maelekezo kwa dada jinsi ya kujaza kuponi.

PIKIPIKI ya tatu kutolewa kesho katika Viwanja vya Bakhresa, Manzese jijini Dar es Salaam tangu kuanza kwa droo ndogo za Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili. Zawadi hiyo itakwenda sambamba na simu za kisasa smatphone, seti ya televisheni na dinner set.

Wananchi wakiendelea kujaza kuponi za Shinda Nyumba.

Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema jijini jana kuwa droo hiyo itachezeshwa katika
viwanja hivyo kuanzia saa nane mchana hadi 12 jioni.

“Maandalizi yote kwa ajili ya shughuli hiyo yamekamilika, tunawaomba wasomaji wetu kuendelea kuhifadhi kuponi zao na kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kwani kama tulivyoahidi, zawadi kemkem zitatolewa na washindi watatangazwa mubashara,” alisema Mkanda.

Droo hiyo ndogo ya tatu itafanyika baada ya mbili za awali, ambapo washindi walipata zawadi kama hizo ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem na Mwananyamala kwenye Viwanja vya CCM Mwinjuma.
Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Risasi, Championi, Amani na Ijumaa Wikienda ni kampuni pekee ya uchapaji magazeti nchini kuwahi kutoa zawadi kubwa ya nyumba katika bahati nasibu.


Ili kupata kuponi hizo, msomaji anatakiwa kununua mojawapo ya magazeti ya kampuni hiyo na kujaza kuponi
zilizopo katika ukurasa wa pili wa magazeti hayo na kuzipeleka kwa mawakala waliopo nchi nzima na kwa wale wa Dar, wanaweza kupeleka ofisi za Global Publishers, zilizopo Bamaga, Mwenge. Bahati nasibu hiyo ya
Shinda Nyumba Awamu ya Pili, imedhaminiwa na British School waliopo karibu na Kituo cha Daladala cha ITV na
Kanisa la Lutheran Mwenge na Kilimanjaro Institute of Technology waliopo Mwenge kwa Mama Ngoma na Sinza
Mori.

Leave A Reply