The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya Kupika Keki ya Karoti

KATIKA safu hii pendwa ya Mapishi, leo tunaangalia jinsi ya kutengeneza keki ya karoti.

MAHITAJI

-Mayai manne

-Siagi kikombe kimoja na robo

-Sukari nyeupe -vikombe viwili

-Vanila vijiko viwili vya chai

-Unga wa ngano vikombe viwili

-Baking powder vijiko viwili vya chai

-Chumvi nusu kijiko cha chai

-Mdalasini vijiko viwili vya chai

-Karoti nne

-Baking soda kijiko kimoja

-Siagi ya maziwa robo tatu kikombe

-Tui la nazi kikombe kimoja

 

 

KUTAYARISHA NA KUPIKA

Washa oven weka nyuzi joto 350

Chukua bakuli weka unga, sukari, baking powder, baking soda, mdalasini, chumvi kisha chang-anya vizuri sana. Weka pembeni.

Chukua bakuli lingine weka mayai, siagi, vanila na tui la nazi koroga mpaka viwe laini kabisa.

Mchanganyiko wenye mayai mwagia kwenye unga kisha koroga mpaka uone vimechanganyikana vizuri.

Chukua karoti ulizoziandaa ukazikwangua weka kwenye mchang-anyiko wako.

Koroga vizuri sana. Chukua chombo unachotumia kupikia keki yako kipake siagi.

Chukua mchanganyiko wa keki, mwagia kwenye chombo hicho, weka kwenye oven.

Dakika 45 zikipita, funua angalia kama keki imeiva. Chukua toothpick ichome katikati ya keki, kikitoka kikavu imeiva. Ikiwa bado irudishe kwenye oven.

Na hapo itakuwa tayari kwa kula.

Comments are closed.