The House of Favourite Newspapers

Aliens wahusishwa na maajabu ya pembetatu ya shetani

0

Scary_Movie_AliensKama nilivyoeleza wiki iliyopita, Bermuda Triangle au Pembetatu ya Shetani ni eneo la uso wa dunia ambalo limekuwa likihusishwa na masuala mbalimbali ya nguvu za kimaajabu. Ni eneo ambalo maelfu ya watu wamepoteza maisha, ndege na meli nyingi zimepotea, pasipo kujulikana zilipokwenda. Bermuda Triangle inapatikana Pwani ya Kusini-Mashariki mwa Marekani na iko katika Bahari ya Atlantiki. SASA ENDELEA…

Yapo mataifa yaliyoamua kuwekeza kufanya utafiti katika eneo hilo lakini walijikuta wakipoteza fedha nyingi bila mafanikio.

Kuna taarifa kuwa zaidi ya ndege na meli 1,000 zimepotea kwa muda wa miaka 500 iliyopita.

Inasemekana kuwa Bermuda Triangle ilitokea baada ya Sayari ya Dunia kugongana na kimondo huko angani miaka 11,000 iliyopita. Mgongano huo ulitokea katika eneo la Bahari la Dunia na kusababisha bahari kuzama kwa futi 10,000 chini ya usawa wa bahari. Kimondo hicho kiliacha mionzi ambayo husababisha ndege kupoteza uelekeo inapofika katika eneo hilo na kuzamisha meli na binadamu.

Inasemekana pia kuwa viumbe waishio angani kama Aliens, huwa wanakaa katika eneo hilo la Bermuda Triangle. Kama nilivyosema awali, viumbe hao wana teknolojia ambayo hukinzana na teknolojia yetu ya duniani, kwa hiyo ndege, meli na binadamu wanapopita eneo hilo huvutwa na kani ya mvutano ambayo ni kubwa sana kutoka kwa wale viumbe waishio katika eneo hilo la Bermuda.

Data zinaonesha kuwa kama ilivyokuwa kwa Area 51, kuna serikali huwa zinajaribia silaha ambazo zinakuwa zimetengenezwa na uangalizi wa silaha hizo. Inaelezwa kwamba, serikali ya Marekani ikishirikiana na Aliens huhusika katika majaribio hayo.

Viumbe hawa wana teknolojia kubwa kiasi cha kukinzana na teknolojia ya duniani na hatimaye kusababisha madhara kwa meli na ndege.

Inaelezwa kwamba, katika eneo hilo kulikuwa na mji wa kale chini ya maji katika Bahari ya Atlantiki ulioitwa Atlantis, mji huo ulikuwa umejengeka kwa barafu ambazo zilikuwa kama kioo ambazo pia zilikuwa ni chanzo cha nishati.

Mji ulisahaulika milele, kwa hiyo  Bermuda iko kwenye huo mji uliozikwa kitambo ambapo kuna kani kubwa ambayo huharibu meli na ndege.

Kuna madai mazito kuwa, Bermuda ni eneo kwa ajili ya maharamia kufanya kazi zao. Maharamia hao ni wale wanaojulikana kwa bendera nyeusi zenye picha ya fuvu.

Lakini dhana hii imeshindwa kuelezea ni kwa nini ndege na meli huwa zinapotea katika eneo hilo kwani wachunguzi wa mambo wamehusisha na utekaji nyara wa meli baharini ambao hufanywa na maharamia hao.

Yapo maandiko yanayoonesha kuwa volkano na gesi ya Methane katika eneo la Bermuda hupunguza mgandamizo wa maji katika eneo hilo na kufanya meli kupoteza uwezo wa kuelea na hatimaye kuzama.

Eneo hili limekuwa likitoa gesi hiyo ya Methane tangu miaka 15,000 iliyopita. Ukungu wenye hali ya ki-elektroniki na sumaku. Ukungu wenye nguvu ya kuzalisha umeme ambapo husababisha dira hupoteza uelekeo na kuwachanganya marubani pamoja na manahodha, hatimaye ndege na meli hizo hupotelea katika Eneo la Bermuda.

Eneo la Bahari ya Atlantiki hasa upande wa Caribbean hukumbwa na kimbunga kikali na mawingu mazito, Bermuda ni eneo ambalo limepakana sana na Caribbean na hukabiliwa na upepo na wingu zito ambavyo husababisha mushkeli kwa ndege, meli na binadamu huku Aliens wakiendelea kupeta kwa raha zao.

Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply