The House of Favourite Newspapers

Penzi la Shumileta lamtesa TX Moshi Jr

0

Moshi William ‘Tx Moshi Jr’, mwimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma.

Brighton Masalu

MAHABA niteketeze! Moshi William ‘Tx Moshi Jr’, mwimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma anaendelea kuwewesekea penzi la aliyekuwa mpenzi wake wa zamani ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, Moshi alisema ingawa kimepita kipindi kirefu tangu atengane na Shumileta, bado analikumbuka penzi la msanii huyo na kwamba alikuwa mwanamke mwema na mwenye kila sifa ya kuwa mke wa mtu na hujutia ni kwa nini alichezea bahati ya kumuoa.

Msanii wa filamu Bongo, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’.

“Dah, unajua nakumbuka mbali sana, hakika Shumileta alikuwa zaidi ya mwanamke, nalikumbuka penzi lake na mara nyingi huwa najutia ni kwa nini nilichezea bahati ya kumuoa mwanamke huyo, bado naumia sana,” alisema Tx Moshi Jr.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply