The House of Favourite Newspapers

Unamtumiaje rafiki mwenye akili darasani

0

studentsKwenye maisha ya kujifunza huwa kuna wanafunzi wa aina mbalimbali ambao wanaweza wakawekwa kwenye makundi mengi iwezekanavyo, lakini kundi muhimu zaidi ni lile linalofuata kigezo cha taaluma ambapo hapa huwa tunaangalia kundi la wanafunzi kwa kipimo cha akili zao darasani.

Katika kundi hili kuna wale wanaojifunza taratibu na wanahitaji jitihada za ziada kujua vizuri mada walizofundishwa na hata ufaulu wao huwa kwa kiwango cha kawaida au hufeli kwenye baadhi ya masomo kutokana na uwezo wao kuwa chini.

Mbali na hao kuna wale wanafunzi ambao uwezo wao wa kujifunza kitu huwa wastani yaani huweza kumsikiliza mwalimu na kuboresha uwezo wao katika mada husika kwa kujisomea wenyewe na kufaulu kwa wastani bila kufeli sana au kufaulu sana.

Kundi jingine ni la wanafunzi wanaojifunza kwa haraka zaidi hawa wana uwezo wa kuelewa upesi mada kutoka kwa mwalimu pindi wanapofundishwa somo fulani na kuweza kuwaelekeza wenzao pasipo hata kujisomea tena hawa ndiyo ambao huwa na ufaulu mkubwa hata kwenye mitihani yao.

Mseto huu wa makundi haya yote matatu hukaa kwa mchanganyiko ndani na hata nje ya darasa yaani unaweza ukakuta mwanafunzi mwenye akili sana darasani, lakini rafiki yake akawa ni yule ambaye hana akili sana darasani, au mwenye akili za wastani.

Lakini cha kushangaza ni kwamba hata yule asiye na akili sana inawezekana kabisa akawa anashindwa kabisa kumtumia rafiki yake huyo kwa ajili ya kuboresha uwezo wake wa kufaulu na badala yake wakaishia kuzungumza mambo mengine ambayo kimantiki hayana faida yoyote kwake.

Sikatai kuwa wapo wengine ambao wanawauliza marafiki zao kuhusu masomo , lakini huenda wakawauliza bila kutilia maanani suala hilo kwa kuwa hawajui umuhimu wa kufanya hivyo japo kuwa kitaalam ni kwamba baadhi ya wanafunzi wanaweza wasiwmuelewe kwa haraka mwalimu kuliko wanapofundishwa na wanafunzi wenzao waliowazoea.

Hiyo inatokana na sababu nyingi lakini kubwa zaidi ni kwamba inaweza ikawa ni njia ngumu za kufundisha zitumiwazo na mwalimu na kuishia kueleweka na wanafunzi wachache pia ukali wa mwalimu unaweza ukasababisha mwanafunzi asielewe vizuri kwa kuwa na hofu.

Leave A Reply