The House of Favourite Newspapers

Faiza ambania Sugu ‘bethidei’ ya mwanaye

0

faiza_ally231Msanii ambaye ni mpenzi wa zamani wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally

Imelda Mtema

Msanii ambaye ni mpenzi wa zamani wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally juzikati alimfanyia mwanaye Sasha pati katika siku yake ya kuzaliwa lakini cha ajabu hakumualika mzazi mwezake huyo.

Sugu na SashaMbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mwanaye Sasha.

Pati hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa Faiza, Mkwajuni jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali ila Sugu hakuonekana eneo hilo.

Baada ya kuiona hali hiyo, mwandishi wetu alimuuliza Faiza sababu za Sugu kutokuwepo kwenye siku hiyo muhimu ya mtoto wao ambapo alisema:

“Unajua yule ni baba halali wa mtoto huyu na katika hali ya kawaida alitakiwa kumtakia hata heri ya kuzaliwa lakini hakufanya hivyo. Nahisi hata hakuwa anakumbuka siku hiyo muhimu ya kuzaliwa mtoto wake sasa mimi nisingeweza kumualika kwa sababu bila yeye maisha yanaendelea.”

Leave A Reply