The House of Favourite Newspapers

Betika Laendelea Kujizolea Umaarufu Kitaa

IKIWA bado ni katika msimu wa Sikukuu ya Pasaka, Gazeti la Betika kama kawaida limeingia mtaani na wasomaji wameendelea kulipokea kwa mikono miwili.

 

Gazeti hilo ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na linaingia mtaani kila Jumatano.

 

Kila linapoingia mtaani, timu ya maofisa masoko wa Global Publishers huzunguka mitaa mbalimbali ambapo leo Jumatano timu hiyo ilitembelea Temeke, Tandika, Mwembe Yanga, Mtoni kwa Aziz Ally na kukutana na wasomaji mbalimbali wa gazeti hilo.

 

Wasomaji waliokutana na timu hiyo ya maofisa masoko, waliendelea kulizungumzia gazeti hilo ambalo ni mahususi kwa masuala ya kubeti.

 

“Gazeti hili limekuja wakati mufaka kwa sisi tunaojihusisha na masuala ya kubeti kwani lina mambo mengi yanatusaidia tofauti na zamani ambapo tulikuwa tunapata shida sana kubeti na kushinda.

 

“Kupitia Betika, tunabeti kwa urahisi na kushinda mara kwa mara, ama kwa hakika gazeti hili ni mkombozi wetu.

“Niwapongeze tu wale wote wanaoliandaa gazeti hili, walifikiria sana mpaka kulianzisha kwani huko nyuma hakukuwa na kitu kama hiki hapa nyumbani, wametusaidia sana,” alisema mmoja wa wasomaji hao.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, naye alisema katika gazeti hilo, kuna nafasi kwa watangazaji kuleta matangazo yao ili kujitangaza.

 

“Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

 

“Bado tunapokea matangazo, hivyo hii ni fursa ya watu ambao wanataka kutangaza nasi kuleta matangazo yao kwetu,” alisema Mgema.

 

Betika lina kurasa 20 za rangi ambapo mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

 

MWANDISHI WETU

Comments are closed.