The House of Favourite Newspapers

D’jaro awashtua mashabiki, hakuwa akilipwa!

0

Djaro Arungu (1)

Djaro Arungu akiwa ndani ya studio za Global TV Online leo.

Djaro Arungu (2)

Djaro Arungu akijibu baadhi ya maswali ya mtangazaji wa Global TV Online (hayupo pichani).

Djaro Arungu (3)

Djaro Arungu akipozi na mtangazaji wa Global TV Online, Shorvieny Mohammed.

Djaro Arungu (4)

Djaro akiwa na mwandishi mahiri wa hadithi na mikasa wa Global Publishers, Azizi Hashim.

Djaro Arungu (5)

Djaro akiwa na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Amran Kaima.

Djaro Arungu (6)

Djaro Arungu akipozi na Patrick Buzohera wa Global TV Online.

MTANGAZAJI maarufu wa Kipindi cha Papaso kinachoruka TBC FM, Djaro Arungu leo ametimba ndani ya Global TV Online na kuwashtua mashabniki wake baada ya kufungukia maisha yake kwamba kabla ya kuanza kutangaza rasmi, hakuwa akilipwa.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Mtu Kati, Djaro ambaye kwa mujibu wa ripoti ya Synovate inamtambua kama mtangazaji anayesikilizwa zaidi nchini alisema kuwa, hapo awali kabla ya kujiunga na Media kubwa nchini kama vile Sahara na nyinginezo alikuwa mpiga picha wa mitaani na hata alipoanza kazi ya kutangaza hakuwa akilipwa.

“Nimepitia maisha magumu sana katika utangazaji hadi kufikia hapa. Nilikuwa mpiga picha mtaani na vilevile sikuwahi kulipwa hata pale nilipoanza kutangaza kwa mara ya kwanza redioni,” alisema Djaro.

Djaro pia alifafanua maana ya kipindi cha Papaso kinachowakutanisha mastaa kibao Bongo na kusema kuwa jina hilo limetokana na neno Papasa ikiwa na maana halisi ya kukitafuta kitu kwa umakini.

(PICHA/STORI: ANDREW CARLOS NA PATRICK BUZOHERA / GPL)

Leave A Reply