The House of Favourite Newspapers

Hispania: Watu 932 Wafariki Ndani Ya Saa 24

0

KWA mujibu wa data zilizotolewa na Wizara ya Afya nchini Hispania  humo leo Aprili 3, 2020, jumla ya watu waliofariki dunia baada ya kuugua #COVID-19 imefikia 10,935.

 

Idadi hiyo imefikiwa baada ya vifo 932 vya wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona kurekodiwa katika saa 24 zilizopita. Jana, wizara hiyo ilitangaza vifo 950 vilivyotokea ndani ya saa 24.

 

Aidha, data za wizara hiyo zinaonyesha kuwa kuna wagonjwa 76,262 kwa sasa nchini humo, ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 2,770 kutokea idadi ya jana lakini pia ni ongezeko dogo tangu Machi 20.

 

Hispania ni moja ya nchi iliyoathirika vibaya na mlipuko wa ugonjwa huu, ikiwa ni ya pili kwa idadi ya vifo nyuma ya Italia yenye vifo 13,915. Inashika nafasi ya pili kwa waathiriki ikiwa na aathirika 117,710 nyuma ya Marekani (245,380).

 

Idadi ya watu walioathirika na maambukizi ya virusi vya #COVID-19 imezidi milioni moja ulimwenguni kwa mujibu wa Chuo Kikuu Cha Johns Hopkins.

 

Nchi tano zenye waathirika wengi waliorekodiwa ni Marekani (245,184), Italia (115,242), Hispania (112,065), Ujerumani (84,794) na China (81,620).

 

Lakini pia nchi tano zenye idadi kubwa ya vifo vilivyoripotiwa ni Italia (13,915), Hispania (10,348), Marekani (6,088), Ufaransa (5,387) na China (3,322).

Leave A Reply