The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Wakipata Madaraka Watatugawa Vipande-Vipande – Video

0

 

MGOMBEA urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli, leo Jumanne, Septemba 22, 2020 ameendelea na kampeni zake za kunadi sera zake kwa wananchi na kusaka kura za uchaguzi mkuu  ujayo.

 

Akizungumza na wananchi wa Igalula mkoani Tabora, Magufuli amesema:

“Ni mara chache sana kukuta watu wamefurika hivi tena asubuhi saa mbili, wenzetu kule wanajua kuchakata, wanatumia picha za miaka ya zamani waonekane wamejaza watu kwenye kampeni zao, waje wajionee kwenye kampeni za CCM watu walivyofurika, hongereni sana.

 

“Nakumbuka nilipita hapa nikapewa madumu mawili ya asali, na ile asali ilikuwa nzuri!  Asali ya huku ni nzuri haloo, ni orijino na ukiinywa unajua umekunywa asali kweli, sishangai hapa mnavyoongezeka na mambo yanakuwa mazuri, asali oyeee!

 

“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliiweka nchi yetu kuwa Taifa moja, hakuna kubaguana, ndiyo maana mpaka leo hatujawahi kupigana wenyewe kwa wenyewe, licha ya makabila mengi lakini tumeunganishwa na lugha ya Kiswahili, maendeleo yote tunayoyafanya ni kwa umoja.

 

“Mmesikia sera za wenzetu, wanasema wakipata madaraka nchi hii wanaiganya vipande-vipande vinavyoitwa majimbo, kila jimbo na Serikali yake, bajeti yake na matumizi yake, nchi hii kila sehemu ina utajiri wake mengine masikini sana, tunaenda wapi?

 

“Tunaingia kwenye siasa za kugawanywa, ukishakata hayo majimbo maana yake hata kiongozi lazima atoke kwenye kabila lililopo eneo hilo, inawezekana awe na dini ya mahali fulani, tunarudi kwenye ukoloni, hata wakoloni walifanya hivi kututawala.

 

“Baadhi ya nchi zimepigana kwa sababu ya majimbo, kuna nchi huko Magharibi, jimbo moja lilitaka kujitenga likidai lenyewe ni tajiri kuliko majimbo mengine, vikaanza vita, suala la majimbo hata kama mimi hamnihitaji, lakini hilo kamwe tusilikubali.

 

“Wengine wanasema ndege hazina faida, mtalii utamleta kwa bodaboda? Lazima aje kwa ndege, ukitaka kusafirisha asali utaipeleka Saudi Arabia au Marekani kwa bodaboda? Tumeshika njia nzuri ya maendeleo na uchumi unapaa ndiyo maana tumefika uchumi wa kati.

 

“Mambo yetu sasa tunayafanya wenyewe bila kutegemea fedha zao, wanashangaa Tanzania inanunua nndege 11? Na mwaka huu tunanunua ndege  tano, reli ya umeme, bwawa la umeme wa megawatt 2,115, umeme utakuwa wa kutosha na mwingine tutauza nchi za jirani.”

 

Leave A Reply