The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Haji Manara Afungiwa Miaka 2 Kujihusisha na Soka, Apigwa Faini Milioni 20

0
                                 Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara

 

BREAKING: Kamati ya Maadili ya TFF imemhukumu Ndugu Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kipindi cha miaka miwili (2) na kutozwa faini ya Tsh. Milioni 20 [Tsh 20,000,000] kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia Adhabu hiyo inaanza leo Alhamisi, Julai 21, 2022.

Haji Manara alipishana kauli ya Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

Kamati ya Maadili ya TFF, imeyataja makosa aliyoyafanya Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara ikiwemo kumtolea maneno machafu Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wa mechi kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa jijini Arusha.

Leave A Reply