The House of Favourite Newspapers

Abdallah Bulembo: Lazima Niiseme Serikali Yangu (VIDEO)

0

Mbunge wa Kuteuliwa, Mh, Abdallah Bulembo akichangia Bungeni jana Tarehe 22/05/2017 kuhusu makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi amesema hatoionea haya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akieleza kuwa ni lazima aseme ukweli kuhusu mambo kadha wa kadha yanayowakumba wavuvi wadogo wadogo pamoja na wawekezaji wa uvuvi ambao wamekuwa hawana tija kwa manufaa na maendeleo ya Taifa.

Katika mchango wake, Bulembo alionesha kushangazwa na Serikali kutoa kibali cha muda wa miaka 20 cha uvuvi kwa mwekezaji kutoka nje ya nchi ambaye amekuwa akileta wafanyakazi wasio Watanzania kwa kuwaajili kama wahasibu lakini baadaye wanaingia baharini na wakifanya kazi ya kuvua samaki ilihali wapo Watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi hizo na hawana ajira.

Aidha Bulembo alieleza namna ambavyo Watanzania wamekuwa wakinyimwa vibali vya uvuvi wakati wageni wanapatiwa.

Leave A Reply