The House of Favourite Newspapers

ACT Wadai Serikali ‘Imekataa’ Ripoti Yake Yenyewe – VIDEO

Chama cha ACT Wazalendo kimeduwazwa na hatua ya Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuikataa ripoti yake yenyewe (Annual Education Sector Performance Report) inayoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu amesema serikali haina sababu za msingi kuikataa ripoti hiyo kwani imetolewa na serikali yenyewe huku akisema ili kuboresha elimu nchini ni lazima Serikali iwekeze kwa walimu na kuboresha miundombinu ya kufundishia.

 

“Ripoti hii kwa kawaida hutoka kila mwaka, hivi karibuni Wizara ya Elimu na Wizara ya TAMISEMI walikutana Dodoma kutathimini mwenendo wa kiwango cha elimu nchini, wakatoka na ripoti Annual Education Sector Performance, cha kushangaza baada ya sisi kuanisha madudu yaliyopo kwenye ripoti hiyo, wakatoka hadharani haraka na kuikanusha.

 

“Wamesema wataitoa kwa umma mwezi Novemba lakini sisi tuliipata kwenye vyanzo vyetu, na inaonyesha kiwango cha wanafunzi wa darasa la pili wanaojua kusoma na kuandika kwa ufasaha kimeporomoka hadi asilimia 49 huku asilimia 6.7 wanafunzi hao wanajua kujumlisha na kutoa,” alisema Shaibu.

VIDEO: MSIKIE ADO SAHIBU AKIZUNGUMZA

Comments are closed.