The House of Favourite Newspapers

Afrika Kusini na Marekani Kuanza Kujaribu chanjo mpya ya ugonjwa wa Ukimwi

0

Afrika Kusini na Marekani zinatarajia kuanza kujaribu chanjo mpya ya ugonjwa wa Ukimwi na tayari wamekwisha anza kuwaandikisha watu kushiriki katika jaribio hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utafiti la Marekani (NIH), chanjo hiyo inayoitwa VIR-1388 imeundwa kusaidia seli za mwili zijulikanazo kama T-cells, seli hizo ni sehemu ya mfumo wa kinga ambazo hukagua seli zenye matatizo.

Chanjo hiyo inafadhiliwa na Shirika la NIH na Bill and Melinda Gates pamoja na Kampuni ya Kimarekani ya Vir Biotechnology.

Jaribio hilo litajumuisha watu 95 ambao hawana ugonjwa wa ukimwi kutoka maeneo manne tofauti nchini Afrika Kusini na maeneo sita nchini Marekani.

Majibu ya kwanza ya jaribio hilo yatatolewa mwishoni mwa mwaka 2024, hata hivyo baadhi ya watu wataendelea kuwepo kwenye jaribio hilo kwa miaka mitatu.

Sehemu ya kwanza ya zoezi hilo itafanya tathmini ya usalama wa chanjo hiyo na uwezo wake wa kushawishi muitikio maalumu wa kinga ya VVU kwa watu.

Mwaka 2020 NIH ilisimamisha jaribio la chanjo nyingine nchini Afrika Kusini baada ya kugundulika kuwa chanjo hiyo haikufaa kuzuia maambukizi ya VVU.

MAREKANI: HOTUBA NZITO ya RAIS RUTO KATIKA MKUTANO wa 78 wa BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA…

Leave A Reply