The House of Favourite Newspapers

Afrika Kusini: Wazungu Waliomuingiza Kijana Mweusi Kwenye Jeneza Wafikishwa Kortini

0
Watuhumiwa wakiwa mahakamani

AFRIKA KUSINI: Wakulima wawili wazungu watafikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini, baada ya kutuhumiwa kuwa walimsukuma kijana mmoja mweusi na kumuingiza ndani ya jeneza akiwa hai, huku wakitishia kumwagia mafuta ya petroli ili wamteketeze kwa moto.

 

Wakati Victor Mlotshwa alipokataa, wakulima hao walimtishia kuwa watamweka ndani ya jeneza hilo pamoja na nyoka.

Mlotshwa

 

Washtakiwa hao Willem Oosthuizen na Theo Jackson, walikamatwa mwezi Novemba 2016, baada ya video ya kitendo hicho kilipowekwa na kusambaa mitandaoni.

Walisema kuwa, Bwana Mlotshwa alipitia kwenye shamba lao liliko katika Jimbo la Mpumalanga, bila ya kuwa na idhini, na walikuwa wakimuadhibu.

Katika kusikizwa kwa kesi hiyo awali, jaji wa mahakama alisema kuwa wakulima hao walikuwa wakatili na waliojaa tabia za ubaguzi wa rangi.

Chanzo: BBC

 

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply