The House of Favourite Newspapers

Akimbiwa na Mumewe Kisa Unene, Hawezi Kutembea – Video

0

MKAZI mmoja mwanamke wa Kijiji cha Mwendakulima, Kata ya Uyoa, Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, amejikuta akishindwa kutembea na hata kufanya shughuli zake kutoka na unene uliopita kiasi (kilogramu 240), hali inayomfanya aendelee kuishi kwa kutegemea msaada kwani mumewe alimkimbia kutokana na unene huo.

 

Bi. Jane Hosea Kalabu ni mama wa watoto sita, amekumbwa na tatizo la mwili kuongezeka kupita kawaida hali ambayo imebadilisha kabisa ndoto za maisha yake ambapo mwaka 2017 alipopima uzito alijikuta akiwa na kilo 240.

 

Mume wake alimkimbiaa kutokana na mwili wake kuongezeka kupita kawaida hali iliyosababisha pia watoto kushidwa kuendelea na masomo.

 

Majirani zake wamejaribu kumsaidia pale walipoweza lakini jitihada zao hazijazaa matunda, zaidi wanaomba serikali kumtazama mama huyu kwa jicho la huruma aweze kupata msaada wa matibabu.

 

 

 

Full Video ipo Hapa

Leave A Reply