The House of Favourite Newspapers

Afya ya Johari yashtua wengi!

0

johaKUNENEPEANA! Na ‘kuumuka’ kwa muigizaji wa muda mrefu, Blandina Chagula ‘Johari’ kumezua gumzo na mishangao kwa wadau wengi wa filamu na burudani huku wakihoji kwa undani mabadiliko hayo ya ghafla kwani siku chache zilizopita Johari alikuwa habari ya mjini kutokana na kudhoofika kwa afya yake.

Wakizungumza na Amani hivi karibuni, baadhi ya mashabiki na wasanii mbalimbali, walionekana kushangazwa na muonekano mpya wa Johari na wengine kufika mbali kwa kuhusisha na madawa maalum ya kunenepesha.

“Mmh, jamani, mbona Johari kanenepeana sana? Si ndiyo kusema maisha yamenyooka zaidi? Lazima kutakuwa na jambo maana siku chache tu alikuwa amekondeana sana, si bure,” alisema mmoja wa wasanii wa filamu ambaye ni moja rafiki wa Johari.

Hata hivyo, ‘kibinubinu’ wetu alimtafuta Johari ili kusikia chochote kutoka kwake juu ya mabadiliko ya mwili wake ambapo kwa haraka alifunguka:

“Duh! Ina maana watu wanashindwa kufuata mambo yao wanabaki kuchunguza mabadiliko ya mwili wangu? Kwa sasa sina stress (mawazo) yoyote nimeridhika na maisha hivyo lazima mwili wangu ubadilike, si kingine zaidi,” alisema Johari.

Leave A Reply