The House of Favourite Newspapers

Jb Ubunge haupo tena moyoni

0

JABKama kawaida ya kolamu hii kuwaletea wasanii mbalimbali na kuwabananisha maswali kedekede ambayo yamekuwa yakiwaumiza vichwa wasomaji wa gazeti hili kwa kushindwa kuelewa undani wake.

Alhamisi ya leo tunaye mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ ambaye amefunguka maswali mbalimbali kama ifuatavyo:

Msomaji: Ni wasanii gani unaowakubali Bongo?
JB: Kutokana na nafasi yangu niliyokuwa nayo katika uigizaji siwezi kulijibu hilo kwa sababu wote wananichukulia kama baba na pia wanafanya kazi vizuri.
Msomaji: Niliwahi kusikia una mpango wa kuwa mbunge, ndoto yako ilifia wapi maana hadi uchaguzi umeisha sijaona ukitangaza nia?

JB: Kifupi ubunge haupo tena moyoni na nimeamua nitulie tu. Sanaa ya uigizaji naipenda kuliko chochote na kwa sasa hata niambiwe niwe rais sitapenda.
Msomaji:Unazungumziaje kuyumba kwa Bongo Movie?

JB: Bongo Movie wala haijayumba ila inatakiwa ipige hatua nyingine, mfano kuna kipindi Bongo Fleva ilionekana haifanyi poa lakini ilipoanza kusikika kimataifa ikaonekana ipo vizuri.

Msomaji: Ilikuwaje ukanyweshwa sumu kaka na umechukua hatua gani hadi sasa kwa wahusika?

JB: Siwezi kusema ni sumu ya kuwekewa kwani bado siamini hivyo, ninachoamini chakula kilikuwa kimelala (kiporo) au labda kiliharibika kwa sababu madaktari hawakuniambia kama nimewekewa sumu walisema nimekula sumu.
Msomaji: Inasemekana wasanii wa Bongo Movie hamna wivu wa kimaendeleo ndiyo maana sanaa yenu haikui kimataifa ni kweli?

JB: Kwa hilo si kweli. Sanaa yetu kwa sasa imepiga hatua kubwa hata nje ya nchi tunatambulika, mfano hata ukiingia katika Mtandao wa Youtube kuna video inaowaonesha Ray na Kanumba wakigombewa nchini Kongo. Huku ni kukubalika.
Msomaji: Unawezaje kulinda ndoa yako kwa vishawishi unavyokutana navyo kutokana na ustaa wako?

JB: Kwanza ieleweke kwamba mimi ni mtu ninayejiheshimu pia ni ngumu sana kuniona kwenye mikusanyiko ya watu labda kuwe na ishu maalum.

Msomaji: Nakupongeza kwa kutokuwa na skendo, unawezaje kujikinga na hilo?
JB: Kutokana na nafasi yangu na heshima kubwa niliyonayo kwenye jamii pia mimi ni mpole tangu mdogo isitoshe ni mtu wa Mungu. Mbali ya yote ni balozi wa kampuni tano na Jumamosi (wiki iliyopita) nilipewa ubalozi wa Kiboko (vifaa vya ujenzi) hivyo bado naendelea kulinda heshima yangu kwa zaidi ya miaka 20 kwenye sanaa.

Msomaji: Bado upo na mkeo? Mmebahatika kupata watoto wangapi? Kwa nini hukupenda kuoa msanii mwenzio?

JB: Niliamua kuoa mtu ninayempenda na sikuwa na haja ya kuoa msanii mwenzangu. Watoto bado hatujabahatika hilo kwangu si tatizo kwani Mungu ndiye anapanga.
Msomaji: Ni changamoto gani ulikutana nayo ambayo ukikumbuka unajuta kuwa staa?
JB: Hakuna changamoto yoyote zaidi ya kuona kama nilichelewa kuingia kwenye sanaa, sababu kwa kipindi hiki tu nilichokuwa ndani ya sanaa nimepata manufaa makubwa, naendesha biashara zangu.

Msomaji: Umejipangaje sokoni?
JB: Nina mpango wa kutoa filamu yangu ya Chungu cha Tatu hivi karibuni, yupo Wema Sepetu, Bi Hindu na wengineo.

Pia baada ya hapo nitatoa Filamu ya Karambati Robo nipo na Diana. Kwa sasa naandaa tamthiliya ndani na nje ya nchi japo bado sijajua nitarushia televisheni gani.

Leave A Reply