The House of Favourite Newspapers

WOMEN’S DAY: Airtel Divas Waja na Hii Kuwashukuru Wanaume Wote!

Airtel Divas:  Mkurugenzi wa Airtel Rasilimali Watu, Bi Stella Kibacha akimshukuru mmoja kati ya wafanyakazi wa kiume wa Airtel , Dunia Yusufu leo walipoadhimisha Siku ya Wanawake Duniani yenye kauli mbiu ‘Balance for better’. Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii.
 Meneja Uhusiano wa Airtel Bi.  Dangio Kaniki akitoa zawadi kwa Edward Mtingwa ikiwa ni ishara ya kushukuru wanaume wote wanaofanya kazi na wafanyakazi wa Airtel ‘Airtel Divas’ 
Mkurugenzi Huduma Kwa Wateja wa Airtel, Bi. Adriana Lyamba,  akitoa zawadi kwa Ezekiel Mwakang’ata kwa lengo la kuwashukuru wanaume wote wanaofanya kazi nao. 
Airtel Divas wakiwa kwenye picha ya pamoja leo Machi 8, 2019 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyobeba kauli mbiu ‘Balance for better’ 

 Meneja Uhusiano wa Airtel Bi.  Dangio Kaniki na Jackson Mbando wakiwa na nyuso za furaha katika Siku ya Wanawake Duniani. 

Akiongoza wanawake wenzie wote (Airtel Divas) katika maadhimisho hayo Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu, Bi Stella Kibacha, alisema “leo ni siku yetu Wanawake, ambapo inaadhimishwa dunia nzima kila tarehe8 Machi.

Lakini style yetu sisi Divas  wa Airtel tumeamua kuwashuru kwa zawadi  mwanaume wote hapa Airtel, ni ukweli kuwa tunashinda nao kila siku wanatuonyesha ushirikiano wa kutosha, hawana ubaguzi tunafanya kazi kwa usawa na kusikilizana, kwa kweli tunawashukuru sana”

Bi Kibacha alieleza kuwa “Mwaka huu kauli mbiu ya siku ya wanawake ni ‘#BalanceforBetter’ ikipambanua mambo mengi kati yao ni kujipanga na kupangilia kila jambo ili kuwa na mafanikio”

“Airte Divas Tumejipanga kisawasawa kuhakikisha kila jambo kazini au nyumbani linakaa sawa kwa manufaa yetu na taifa kwa ujumla” alimaliza kwa kusema Bi Kibacha,

#AIRTEL #DABODATA #NASMATIKA

 

Comments are closed.