The House of Favourite Newspapers

Airtel Money Yazindua “Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia”

0
Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda

KAMPUNI ya simu za mkonoini ya Airtel Money Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money imezindua kampeni maalum itakayojulikana kama Aitel Money Tunakuunganisha na Dunia ambapo itawawezesha wateja wote Airtel Money kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya 200 duniani moja kwa moja kupitia akaunti zao za Airtel Money.

Akizungumza jijini Dar wakati akizindua huduma hiyo Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema huduma ya kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya 200 itajulikana  kama Airtel Money Tunakuunganisha na Dunia.hakuna mipaka wala changamoto ya kupokea fedha kutoka nje ya nchi ukiwa na Airtel Money sasa.

“Huduma hii inadhihirisha dhamira ya kuendelea kushirikiana na serikali ili kuleta suluhisho la huduma za kifedha hapa nchini ili kuwafikia Watanzania wengi ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki.

Mkurugenzi Nchunda (kushoto) akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi huo.

“Tunaelewa kwamba tunao ndugu jamaa na marafiki walio nje ya nchi ambao wangependa kutuma fedha kwa ndugu zao wa Tanzania lakini wamekumbana na vikwazo kutokana ha hatua nyingi zinazotakiwa”. Alisema Nchunda.

Mkurugenzi Nchunda aliwasisitiza wananchi wote kuanza kutumia huduma hizo kwa kurahisishia mfumo wa kupokea pesa kirahisi na kuacha kuendelea kuhangaika na njia za kizamani.

Leave A Reply