The House of Favourite Newspapers

Ajib mchezaji bora wa mwezi Simba

0

Ibrahim-Ajib

Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajib.

Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Ajib ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa timu hiyo kwa mwezi Desemba.

Tuzo hiyo aliyoshinda Ajib huambatana na kitita cha Shilingi 500,000 baada ya kufunga mabao matano mwezi uliopita na kuisaidia klabu hiyo kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.

Kwa sasa Ajib anakosekana Simba SC kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita, kufuatia kugongwa na nahodha wa zamani wa Wekundu hao wa Msimbazi, Henry Joseph.

Ajib ni mmoja ya wachezaji wanaopigiwa rada na Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, kwenda kufanya majaribio.

Hadi sasa waliokwenda kwenye majaribio ni Mshambuliaji Haruna Chanongo na beki Abuu Ubwa wa Stand United.

Leave A Reply