The House of Favourite Newspapers

Akilimali: Zesco Tunawachapa Bao Tatu

KATIBU wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa, ana uhakika wa timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa mabao si chini ya matatu watakapocheza dhidi ya Zesco ya Zambia, kesho Jumamosi.

 

Kauli ya Mzee Akilimali inakuja wakati Yanga ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Zesco katika mchezo wa kwanza wa Hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa kwenye Uwanja Mzee  Dar es Salaam wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Mzee Akilimali ameliambia Championi Ijumaa kuwa: “Tayari nimeshaona tuna uwezo mkubwa wa kumfunga Zesco hapa nyumbani. “Kuna kijana wangu ambaye alifanya mambo katika mechi iliyopita dhidi ya Township Rollers, ndiye aliyeniambia kwamba pia Zesco tutawatoa, tena kazi inamalizika hapa nyumbani.

PART 1: HALI Ya Mzee AKILIMALI, Aelezea UGONJWA Wake, Amtaja KIKWETE – “ZAHERA Kanilipia PESA”

“Jumamosi tunamfunga si chini ya mabao matatu na tukienda kule kwao matokeo ya sare yatakuwa na faida kubwa kwetu.

 

“Nasema hivyo kwa sababu nina kijana wangu wakati tunakwenda kucheza na Township Rollers kule kwao, nilimwambia afanye mambo ili tupate sare ya 2-2 tusonge mbele au tushinde 1-0. Akaona matokeo ya 1-0 ni sahihi kwetu, na kweli tukashinda. Watu waende uwanjani Jumamosi washuhudie ushindi huo.”

 

Baada ya mchezo huo, timu hizo zinatarajiwa kurudiana wiki mbili zijazo ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo na atakayepoteza, ataenda kucheza mechi za mtoano katika Kombe la Shirikisho Afrika kusaka nafasi ya kuingia makundi kwa upande huo.

Comments are closed.