The House of Favourite Newspapers

MCHEKESHAJI MARTHA AZIKWA LEO KINYEREZI JIJINI DAR -VIDEO

MWILI wa mchekeshaji (Stand Up Comedian) aliyepata umaarufu kupitia Kipindi cha Cheka Tu kinachoongozwa na Coy Mzungu, Boss Martha umezikwa leo Kinyerezi jijini Dar es Salaam baada ya kufanyiwa ibada nyumbani kwao Kivule.

Mchekeshaji huyo amefariki wiki hii jijini Dar es Salaam ambapo imeelezwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa uti wa mgongo uliosababisha malaria kali na kupelekea kifo chake.

Marehemu ameacha mtoto mmoja aliyezaa na Msanii wa Bongo Fleva, Mbosso ambapo kabla ya kifo chake, walidumu kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka mitano.

Bwana ametoa na bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

 

Comments are closed.