The House of Favourite Newspapers

Akon Akutana na Rais Museveni, Ataka Kuwekeza Uganda

0

MWANAMUZIKI mashuhuri na mzaliwa Senegal ambaye pia ni raia wa Marekani mwekezaji na mhisani Aliaune Damala Badara Thiam, maarufu Akon aliwasili Uganda siku ya Ijumaa Aprili 2, asubuhi kwa ziara ya kibiashara.

 

Hii inafuatia ziara ya hivi karibuni ya mkewe, Bi Rozina Negusir mnamo Januari mwaka huu.

 

Bi Negusir alikutana na Rais Museveni na wakajadili miradi tofauti ya uwekezaji ambayo inaweza kufanywa, kulingana na Wizara ya Mambo ya nje.

 

Akon alipokelewa na Bwana Abbey Walusimbi, mshauri mwandamizi wa rais katika maswala ya ya raia walio nje ya nchi hiyo , mwanamuziki Eddie Kenzo, maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya nje, Bodi ya Utalii ya Uganda, na Sheik Ramadhan Mulindwa kutoka Baraza Kuu la Waislamu la Uganda.

 

Mwaka 2018 Akon alitangaza mpango wa kujenga jiji la kisasa kwa kima cha dola bilioni 6 nchini Senegal kwa jina “Akon City”.

Mradi huo unaoungwa mkono na serikali ya Senegal utakuwa na hoteli za kifahari za watalii ,studio za muziki ,maduka makubwa ya bidhaa na vivutio vingine.

Leave A Reply