The House of Favourite Newspapers

Albamu Mpya ya Burna Boy Inatengenezwa na P Diddy

0

Star wa Muziki wa Nigeria, Burna Boy anajiandaa kuileta album yake mpya “Twice as Tall” na ameweka wazi kuwa album hiyo itaandaliwa na mkongwe wa muziki nchini Marekani, Diddy.

 

Kwenye mahojiano na ‘The New York Times‘ ameweka wazi kuwa Diddy ndio mpishi mkuu wa album hiyo akielezea kuwa album hiyo imerekodiwa kipindi ichi cha Corona hivyo iliwalazimu kuiandaa wakiwa sehemu tofauti.

 

Ameweka wazi kuwa sauti ya Diddy itasikika kwenye baadhi ya ngoma na pia amechangia kuongeza wakali wengine kama Anderson Paak na Timbaland.

 


Burna Boy pia ameweka wazi tarehe ambayo ataiachia album hiyo, tarehe 14 Augosti na itakuwa na mikwaju 15 akiwa amewashirikisha wakali wengine kama Naughty by Nature, Sauti Sol, Youssou N’Dour, Chris Martin na wengine.

 

Leave A Reply