ALBUM YA BEYONCE YAINGIZA MAMILIONI YA MKWANJA

MWANAMUZIKI staa Mmarekani,  Beyonce,  siku kama ya leo, Aprili 24, 2016, aliachia albam yake ya sita ya  Lemonade kupitia mtandao anaomiliki  mume wake wa TIDAL.   Albam hiyo ilishika nafasi ya kwanza miongoni mwa zenye mauzo makubwa duniani mwaka 2016 — ikiuza kopi milioni 2.5 na kwenye mitandao ilitengeneza zaidi ya Dola milioni 8 kwa kusikilizwa na ‘kudownloadiwa’.

Beyonce aliandika na kutayarisha kila wimbo, na msanii wa Rae Sremmurd (Swae Lee) alisaidia kuandika single ya ‘Formation’, Lemonade ilikuwa ni albam ya video tu na ndiyo maana ilitoka kwenye TIDAL kwanza.  Stori ya albam hii ilitoka kwa bibi yake Beyonce na bibi yake JAY Z.
Loading...

Toa comment