The House of Favourite Newspapers

Alichokisema Balozi Mahiga Baada ya Kuapishwa – VIDEO

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi ameanza kazi rasmi kwa kumtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuanza mabadiliko wizarani hapo.

 

Profesa Kabudi ambaye hata hivyo hakusema ni mabadiliko ya aina gani yanahitajika wizarani hapo, amesema hayo leo Jumatatu Februari 4, Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuapa kuwa waziri wa wizara hiyo baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli, juzi.

 

“Lazima tubadilike na tutambue mabadiliko haya ni sisi wenyewe ndani ya wizara na ni mabadiliko ya haraka, huo ndiyo ujumbe wangu na ahadi yangu kwa watu wote,” nchi yoyote lazima itafute nafasi katika Jumuiya ya Kimataifa. Kwa bahati nzuri, nafasi yetu ndani ya Jumuiya ya Kimataifa ipo vizuri na tuna marafiki wengi. Hatuna adui duniani.

 

Tumekuwa na malumbano ya wazi na Mashirika ya Kimataifa, kwa juhudi za Wizara wamenza kutuelewa. Nilipata mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, aliniambia amenipa jukwaa la kueleza uhalisia. Ufaransa pia walinialika na niliwaeleza wakaelewa,” amesema Mahiga.

 

Pamoja na Profesa Kabudi, pia Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Augustine Mahiga aliapishwa na baadhi ya Makamishna wa Jeshi la Polisi.

Comments are closed.