The House of Favourite Newspapers

ALIKIBA KUMDONDOSHA YVONNE CHAKACHAKA

KING wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka kwamba atafanya shoo mbili za kufanga mwaka jijini Dar es Salaam ambapo atakuwa na muimbaji mkongwe, Yvonne Chakachaka kutoka Afrika Kusini.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba ameandika;

“Ikiwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa namshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki katika kila jambo na namshukuru kwa kunipa mashabiki wanaonipa support ya dhati kabisa. Shukrani zangu kwa mashabiki mwaka huu katika Funga mwaka na King Kiba zinakuja na show mbili kubwa ndani ya Desemba 2018.

 

1st Edition ya Funga Mwaka Na King Kiba nitakuwa na Princess of Africa Mama Yvonne_ ChakaChaka itafanyika Serena Hotel Dar es Salaam 22. December. 2018. Halafu 2nd Edition ya Funga Mwaka Na KingKiba itatukutanisha pale Next Door Arena, Dar es Salaam tarehe 29. December.2018.”

 

Nyimbo za Yvonne zilizotamba ni pamoja na I’m Burning Up, Thank You Mister DJ, I Cry for Freedom, Makoti, Motherland, Umqombothi na nyinginezo.

DIAMOND Afunga Mitaa Iringa/Mashabiki Walilia Kusukuma Gari Lake!

Comments are closed.