The House of Favourite Newspapers

Alikiba nje msimu mzima

Ally Saleh Kiba ‘Alikiba’

MSHAMBULIAJI wa Coastal Union ya Tanga, Ally Saleh Kiba ‘Alikiba’, anaweza asionekane uwanjani hadi msimu huu wa Ligi Kuu Bara 2018/19 utakapomalizika.

 

Kiba tangu asajiliwe Coastal Union, amefanikiwa kucheza mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar, KMC kwa dakika chache na amekuwa akihudhuria mazoezi na kambi ingawa siyo mara zote.

Nyota huyo kwa sasa yupo bize na majukumu yake ya kimuziki ndani na nje ya nchi, hivyo amekuwa nje kwa muda ndani ya timu ingawa ni sehemu ya makubaliano naye.

 

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda amesema ni muda mrefu Alikiba hajaonekana katika timu kutokana na majukumu mengine aliyokuwa nayo na mpaka sasa hawajui atajiunga na wenzake lini.

 

“Sijui ataungana na wenzake lini kwa sababu hayupo hapa kwa muda mrefu akiwa na majukumu mengine kama mnavyofahamu kazi yake. “Pengine anaweza asionekane hadi msimu huu unamalizika,” alisema Mgunda. Alikiba aliyejiunga na timu hiyo msimu huu, mpaka sasa amefanikiwa kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara.

SPOTI HAUSI: Sababu Zilizowatoa SERENGETI BOYS Kwenye AFCON!

Comments are closed.