The House of Favourite Newspapers

Aliyekuwa spika wa bunge Afrika kusini ashtakiwa kwa tuhuma za ufisadi

0
Aliyekuwa spika wa bunge Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula akiwa mahakamani huko Pretoria.

Nosiviwe Mapisa-Nqakula, ambaye alijiuzulu wadhifa wa uspika Jumatano, alifikishwa mahakamani mjini Pretoria baada ya kufika polisi na kukamatwa rasmi.

“Mashtaka dhidi ya Bi Mapisa-Nqakula ni makosa 12 ya rushwa na moja la biashara haramu ya fedha,” Bheki Manyathi wa Mamlaka ya Taifa ya Kuendesha Mashtaka ameiambia mahakama.

Akiwa amevaa nguo ya manjano na bluu iliyofanana na kitambaa chake cha kichwani alikaa kizimbani, mwanasiasa huyo mkongwe wa ANC alikaa kimya. Mahakama imekubali ombi la wakili wake kutaka aachiliwe kwa dhamana.

Hili likitokea chini ya miezi miwili kabla ya uchaguzi wa taifa, kesi imeongeza wasi wasi kwa ANC, ambayo inajitahidi kujiweka vizuri katika ukusanyaji maoni huku uchumi dhaifu na shutuma za rushwa kwa afisa na utawala mbaya.

Mapisa-Nqakula ni mmoja wa mwanasiasa mwandamizi wa karibuni wa ANC, akiwa pamoja na rais na makamu wa rais, kukumbwa na kashfa za rushwa.

WAZIRI SILAA AWAJIBU WANAOSEMA ANAINGILIA MAHAKAMA -AELEZA MADUDU YANAYOFANYWA na MATAPELI wa ARDHI

Leave A Reply