The House of Favourite Newspapers

Aliyempa Kibendi Amber Lulu Afunguka

0

 

KUMEKUWA na sintofahamu kubwa kuhusu uwepo wa ujauzito kwa msanii wa Bongo Fleva, Amber Lulu, na stori za mitandaoni zinadai alikuwa na mahusiano na Uchebe na P Funk Majani kwa hiyo mmojawapo huenda akawa mhusika wa ujauzito huo.

 

Msanii wa zamani wa kundi la BOB, Micharazo, ambaye ndiyo anadaiwa kumpa ujauzito msanii huyo, amefunguka na kusema bado haijawa rasmi kuzungumzia suala hilo ila yote ni mipango na baraka za Mungu.

 

Akifunguka zaidi kuhusiana na hilo, Emba Bosion, amesema: “Nisingependa niongelee rasmi hilo suala, Amber Lulu mwenyewe ndiye atanyoosha, hizo zote ni baraka za Mwenyezi Mungu, Inshaalah na Mungu mkubwa.”

 

Emba Bosion ambaye ametoka nyuma ya nondo kwa sasa ni msanii anayepata usaidizi wa kimuziki chini ya Q Chief na tayari ameachia kazi mpya inayoitwa ‘Nyota’, akimshirikisha Billnass na Q Chief.

Leave A Reply