The House of Favourite Newspapers

ALIYETAJWA NA JPM KUIIBIA SERIKALI SH MIL. 7 KWA DAKIKA AACHIWA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli akidaiwa kuiibia Serikali takribani Shilingi milioni 7 kwa dakika, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake wanne.

Yusufali na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif wanakabiliwa na mashtaka 198 ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Tsh bilioni 15.

 

Wakili Mkuu wa Serikali, Hashim Ngole amedai mahakamani hapo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea nalo dhidi ya washtakiwa hao.

 

Kwa upande wake, Hakimu Augustina Mmbando amesema shauri hilo lilikuja chini ya kifungu namba 91(1) cha CPA, sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

 

Hakimu Mmbando amesema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo lakini hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kurudishwa mahabusu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka mengine mahakamani hapo.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.