The House of Favourite Newspapers

Aliyetunga na Kuimba #Jerusalema “Sijalipwa Hata Senti”

0

MWIMBAJI wa ngoma ya ‘Jerusalema’, Nomcebo Zikode amedai kujipanga kwenda mahakamani kudai haki yake kwa kuwa tangu wimbo huo uliojiozolea umaarufu duniani kutoka mwaka jana, hajawahi kulipwa chochote.

 

Nomcebo ambaye alishirikiana na Master KG katika wimbo huo wenye watazamaji milioni 421 kwenye mtandao wa Youtube, kupitia ukurasa wake wa instagram amedai kuwa hajawahi kulipwa hata senti moja wakati Master KG na lebo ya Open Mic wakijizolea mabilioni.

 

Mbali na sauti yake kwenye jerusalema, Nomcebo pia aliandika wimbo huo pamoja na Master KG.

“Asante kwa mashabiki wote wa Jerusalema mmefanya ndoto zangu kuwa za kweli, kwa kupata wimbo maarufu ulimwenguni. Sauti yangu na mashairi yamepita ulimwenguni, lakini bado nasubiri kile kinachostahili kwangu”, aliandika Nomcebo.

 

“Upendo na msaada kutoka kwa mashabiki wa #Jerusalema umekuwa nguvu yangu hasa wakati huu mgumu. Mimi, kama msanii wa kike, siwezi kukaa kimya tena juu ya hili, suala sasa liko kwa mawakili wangu,” alisema.

 

Ikumbukwe kuwa ngoma hii ilipata mafanikio makubwa na kuweka rekodi mbalimbali duniani ikiwemo kuweka rekodi ya kutafutwa zaidi duniani kwenye mtandao wa #Shazzam.

 

Stori: Mushi Gabriel

 

Leave A Reply