The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu Amtamani Jux

0

MSANII wa muziki Bongo, Amber Lulu amesema amepanga kuzaa watoto watano ambapo kila mtoto atakuwa na baba yake.

 

Lulu amesema hayo akidai kwamba sababu kuzaa kila mtoto na baba yake ni kwamba akizaa na baba mmoja kisha baadae akifariki yeye ataishia kupata tabu mwenyewe na watoto.

 

Aidha, mrembo huyo amemtaja msanii Juma Jux kuwa ndio mwanaume anayetamani kupata naye mtoto kwa sababu ana akili, yupo smart na atamuongoza vyema pia amekuwa akimfuatilia msanii huyo kwa muda mrefu.

 

Ikumbukwe pia Lulu mwenye vituko vya rejareja kipindi cha nyuma alishaweka wazi kutamani kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz, lakini hata hivyo haikuwa rahisi na tayari Diamond ameshazaa watoto 4 na wanawake tofauti.

Leave A Reply