The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu: Atakayenioa Atasimulia Dunia Nzima

0

 

MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ amesema kuwa mwanaume atakayebahatika kumuoa atakuwa amebahatika na ikiwezekana anaweza hata kusimulia dunia nzima.

 

 

Akizungumza na AMANI, Amber alisema kuwa yeye ni mwanamke wa tofauti na wanavyomchukulia kwenye mitandao ya kijamii au akipanda jukwaani na kucheza.

 

 

“Lakini ukweli ni kwamba mume wake atapata raha sana kwasababu mwanamke kama mimi ni wachache sana katika dunia hii. “Unajua watu wananichukulia tofauti sana lakini ukweli ni kwamba hakuna mwanamke ambaye anaweza kunikaribia ninapokuwa mke.

 

 

“Yaani staa yeyote hawezi kuwa kama mimi hata kidogo, maana navaa uhusika wa mke anayestahili kuwekwa ndani na mwanaume hivyo nawashauri waoaji wasinichukulie tofauti, mimi ni mke wala sifai kuwa mchepuko” alisema Amber Lulu, ambaye anatamba na nyimbo zake kama jini kisirani na watakoma.

Stori: Imelda Mtema

 

 

Leave A Reply