The House of Favourite Newspapers

Amuua Mkewe Baada ya Kumfumania na Njemba Ndani Kwake

0

 

Peshi la Polisi  mkoa wa Mwanza linamshikilia mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Pastory Majura mwenye umri wa miaka 52, Msukuma,  kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumpiga na kitu kizito kichwani baada ya kumfania akiwa na mwanamume mwingine ndani ya nyumba yake.

 

Taarifa ya jeshi la polisi kupitia kwa Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne, inadai kuwa, Aprili 10, 2020 majira ya 04:00hrs alfajiri, huko kijiji cha Nyamanga, Kata ya Ukara, wilayani Ukerewe, Pastory Majura, alimuua mkewe aitwaye Anusiata James, miaka 52, Mzinza, mkazi wa Kijiji cha Nyamanga, kwa kumpiga kichwani na kitu kizito baada ya kumfumania mke wake nyumbani kwake akiwa na mwanaume mwingine ambaye alikimbia baada ya mtuhumiwa kumkuta nyumbani kwake.

 

Hata hivyo, mume wa marehemu ambaye kwa sasa ni mtuhumiwa, mara baada ya kumshambulia na kumuua mkewe aliamua kujichoma tumboni na kitu chenye ncha kali ambapo alipata maumivu makali na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe kwa matibabu.

 

Upelelezi wa shauri hili unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo. Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

 

MULIRO- ACP

Na Johnson James -GPL

Leave A Reply