The House of Favourite Newspapers

Ang’atwa na Nyoka Sehemu za Siri Akijisaidia

0

SIRAPHOP MASUKARAT  (18), raia wa Thailand, majuzi aling’atwa na nyoka sehemu za siri wakati akijisaidia chooni. Amesema nyoka huyo alitokea kwenye tundu la choo.

“Nilikuwa natumia choo nikaanza kuhisi maumivu sehemu zangu za siri, kuangalia nikamwona nyoka, jambo lililofanya niwahishwe hospitali haraka,” amesema.

Kijana huyo wa kiume alishtuka na kutazama chini ya choo na kumwona chatu aliyekuwa ameuuma kwenye uume wake.

 

Siraphop anasema alipiga mayowe wakati wa tukio hilo ambalo lilitokea huko Nonthaburi, eneo la katikati nchini  Thailand, kiasi cha kilomita 20 kaskazini mwa jiji la Bangkok.

Mara moja alikimbizwa hospitali ya Bang Yai alipopatiwa matibabu ambapo alishonwa nyuzi tatu katika jeraha lililokuwa sehemu ya mbele (ncha) ya uume wake na kusafishwa na dawa maalum za kuua bakteria ambazo zingeweza kusababishwa na meno ya nyoka huyo.

 

Tukio hilo, kwa mujibu wa Siraphop, lilisababisha damu kuenea katika eneo hilo la choo.

 

Kikosi cha kukamata wanyama kilifika katika jengo hilo la ghorofa mbili na kumkuta chatu huyo mwenye urefu wa kiasi cha mita moja akiwa bado chooni hapo wakamkamata na  kumpeleka porini ambako walimwachia.

“Najua nyoka huyo alimjeruhi mwanangu, lakini nashukuru chatu ni nyoka wasiokuwa na sumu,” alisema mama wa kijana huyo ambaye naye alishangaa nyoka huyo alifikaje nyumbani mwao.

Leave A Reply